Bei Mpya za Mafuta Zatangazwa...Zisome Hapa

 


Kwa Mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara), bei za rejareja za Machi 2023 kwa mafuta ya petroli na dizeli yanapungua kwa shilingi 64/Lita na shilingi 209/lita, mtawalia, ikilinganishwa na toleo la tarehe 1 Februari 2023, kutokana na kuisha kwa mafuta ya taa kwenye matanki ya kuhifadhia yaliyopo Tanga,


“Waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kaskazini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika bandari ya Dar es Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika”


“Kwa Mikoa ya Kusini (Mtwara, Lindi, and Ruvuma), bei za rejareja za Machi 2023 kwa mafuta ya petroli zinaongezeka kwa shilingi 138/lita wakati bei ya mafuta ya dizeli zinapungua kwa shilingi 68/lita”


“Kwakuwa hakuna matanki ya kuhifadhia mafuta ya taa katika bandari ya Mtwara, waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kusini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika bandari ya Dar es Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad