Baada ya kuwa kimya ulingoni tangu mwaka jana alipochapwa kwa TKO na Liam Smith nchini Uingereza, bondia Hassan Mwakinyo kupanda tena ulingoni mwezi Aprili mwaka huu. Ameliambia Gazeti la Mwanaspoti.
Bondia huyo mwenye nyota tatu sasa amesema Aprili mwaka huu mashabiki wake watamuona tena ulingoni mjini Dodoma.
“Nitacheza Dodoma na bondia kutoka nje ya nchi, naamini litakuwa ni pambano langu bora na kubwa litakalonirudisha kwenye renki.” ameeleza Mwakinyo.
Mwakinyo ambaye aliwahi kuingia kwenye 20 bora ya dunia kwenye uzani wa Super Welter na namba moja nchini kwenye kila uzani ‘Pound For Pound’ ameporomoka kote na sasa ni wa pili nchini na wa 66 duniani.