Bondia Mwakinyo kuzichapa na Mwafrika Kusini Aprili 23 Dodoma




BONDIA wa Kimataifa, Hassan Mwakinyo amesema amejiandaa vizuri kupigana na bondia mwenzake wa Afrika Kusini huku akiahidi mchezo mzuri wa kuvutia.

Amesema kwa sasa anaendelea kujifua kwa lengo la kuonyesha mchezo nzuri siku hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwakinyo aliiomba Serikali kuunga mkono pambano hilo pamoja na mchezo wa ngumi kwa ujumla ili mabondia wa Tanzania waweze kufanya vizuri kimataifa.


Mkurugenzi wa Kampuni ya Lady in Red Boxing Promotion, Sophia Mwakagenda, akizungumza waandishi wa habari kuhusu pambano la Bondia Hassan Mwakinyo na Bondia Kuvesa Katembo kutoka nchini Afrika ya Kusini litakalofanyika Aprili 23, kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma kwa ajili ya kuchangisha fedha za kununua taulo za kike 40,000 kwa wanafunzi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
“Nimejipanga kufanya vizuri kushinda katika pambano hili, wadau na mashabiki zangu wategemee kuona mchezo nzuri kutoka kwangu,” alisema Mwakinyo.

Mwakinyo alieleza kuwa ni jambo kubwa kuwwapo kwa mgeni rasmi Waziri wa Mkuu, ni jambo ambalo litampa nguvu ya kupambana dhidi ya mpinzani wake.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la kampeni ya kuchangia  taulo za watoto wakike.

Pambano hilo litafanyika Aprili 23, mwaka huu, mkoani Dodoma huku maina card atacheza mtanzania, Hassan Mwakinyo dhidi ya Kuseva Katembo kutoka Afrika Kusini.

Mwakinyo na Katembo watacheza pambano lisilo la ubingwa raundi 10 uzito wa Kati.

Awali, akizungumza kwenye Promota wa pambano hilo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lady in Red Promotion, Sophia Mwakagenda alisema fedha zitakazopatikana katika pambano hilo zitasaidia kununua taulo za kike.

“Fedha hizi tutanunua taulo za kike kwa kusaidia mabinti wetu katika mikoa ya Njombe, Mbeya, Ruvuma na Iringa,”alisema.

Alisema baadhi ya wabunge watacheza pambano kama kuleta hamasa siku wakiwemo Msukuma atacheza na Januari Makamba huku Hamisi Take ‘Babu Tale’ atapimana nguvu na Kingu.

“Wabunge wameniahidi kushirikiana na Mimi katika pambano hili, ndiyo maana siku hiyo watacheza katika raundi tatu kila moja, ” alisema.

Pamoja na pambano la Mwakinyo kutakuwa na  mapambano ya utangulizi matano ambayo ni Jesca Mfinanga dhidi ya Salma Ally, Feriche Mashauri atapimana na Rukia Nasirite  huku Halima Bandola atapigana na Sarafina Julius.

Wengine Happy Daudi atapigana na Hawa Stanford na Yonas Segu atapimana nguvu na Ibrahim Majibu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad