Bodi ya Wadhamini ya HADEMA imeieleza mahakama kuwa imetafakari kwa makini nakuona kwamba hawatakuwa na maswali ya dodoso kwa wabunge wa Viti Maalum, Halima Mdee, Ester Bulaya na Esther Matiko kutokana na kesi waliyofungua ya kuvuliwa uanachama.
Mdee na wenzake 18 walifungua kesi hiyo namba 36/2022, mahakamani kupinga uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama, wakidai kwamba uamuzi huo ulikuwa kinyume Cha Sheria Kwa kuwa ulikuwa wa upendeleo na hawakupewa nafasi ya kusikilizwa.
Taarifa hiyo imewasilishwa na Wakili wa Chadema, Hekima Mwasipu mbele ya Jaji Cyprian Mkeha wa Mahakama Kuu, Masjala Kuu, jijini Dar es Salaam wakati Mbunge Jesca Kishoa akitarajia kumaliza kujibu maswali ya dodoso ya mawakili wa Chadema.
Kutokana na maagizo ya mahakama kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena tarehe 9 na 10 ya mwezi huu