Kwa mujibu wa AFP, Mkataba utaziwezesha Nchi hizo kufanya Miamala mikubwa ya Kibiashara na Kifedha moja kwa moja, Kubadilishana Fedha (#Yuan) kwa Reais ya Brazil bila kuihusisha Dola ya Marekani
Taarifa ya Mamlaka ya Kukuza Biashara na Uwekezaji ya Brazil (ApexBrasil) imesema inatarajia uamuzi huo utapunguza gharama na kukuza Biashara kubwa zaidi pamoja na kuwezesha Uwekezaji
Hatua hiyo inafuatia ushirikiano mwingine ulioripotiwa hivi karibuni na unaoundwa na Nchi za #China, Russia, Saudi Arabia na Iran kwaajili ya kufanya #Biashara kwa kutumia Sarafu za Nchi hizo na kuachana na matumizi ya Dola ya Marekani