Burna Boy anakuwa muimbaji wa kwanza tokea nchini Nigeria na msanii wa pili baada ya Diamond Platnumz kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara kufikisha zaidi ya views bilioni 2 kwenye mtandao wa YouTube.
Kupitia video yake mpya ya Rollercoaster aliyomshirikisha J Balvin yenye zaidi ya watazamaji milioni 4.5 ndani ya siku nane, inamfanya Burna Boy kufikia jumla ya watazamaji Bilioni 2.001 kwenye mtandao wake wa YouTube ndani ya kipindi cha muda wa miaka 5 tangia 2018, nyuma ya Diamond Platnumz aliyefikisha idadi ya watazamaji Bilioni 2 mwishoni mwa mwaka jana, 2022 ambapo hadi sasa ana zaidi ya views Bilioni 2.115 ndani ya kipindi cha miaka 11 na miezi 9.
Ukitazama Speed ya WaNigeria kwenye mtandao wa YouTube, wanaipelekea moto Rekodi ya Diamond ya kuwa ndiye kinara wa wasanii walioko chini ya Jangwa la sahara wenye idadi kubwa ya watazamaji kwenye mtandao huo, na inatishia na kutupa taswira kuwa muda si mrefu atapokonywa utawala huo.
Mfano Speed ya Rema ambaye ana miaka 4 pekee kwenye game, tayari ameshafikisha zaidi ya watazamaji Bilion 1 YouTube, lakini ndiye aliyekuwa mwenye zaidi ya wimbo mmoja katika list ya wasanii 10 barani Afrika ambao nyimbo zao zimefanya vizuri zaidi kwenye mtandao huo mwaka 2022, huku Diamond akikosekana kwenye Top 10 hiyo, wimbo wake uliofanya vizuri zaidi ukiwa ni Watasubiri Ft Zuchu, (22M👁) kwa muda huo.
Kuna Mahala tumekwama🤔