Fatma Karume "TFF Inamlazimisha Fei Toto Aichezee Yanga"



Fatma Karume "


Fatma Karume ambaye ni Mwanasheria wa mchezaji wa Klabu ya Yanga, Feisal Salum (Fei Toto) amesema Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linamlazimisha mchezaji huyo kufanya kazi na Yanga wakati ni kinyume na sheria za FIFA.

 

Mwanasheria huyo amesema TFF ilipaswa kujiuliza ikiwa mchezaji huyo alivunja mkataba kwa njia sahihi au la, na kama hakutumia njia sahihi alipaswa apigwe faini na si kulazimishwa kuitumikia klabu hiyo.

 

“Sheria za FIFA zinasema kwamba ukivunja mkataba kinyume na makubaliano unapigwa faini, na unapigwa faini ili kuifidia timu na ili kuwafundisha wachezaji wengine wasifanye hivyo tena," amesema.

 

 Aidha, amesema ikiwa mchezaji huyo atasimamia msimamo wake wa kutoendelea kuichezea klabu hiyo, atamshauri aende katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS).

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad