Haaland huenda akaikosa mechi ya Man City vs Liverpool Jumamosi hii



Erling Haaland hakuwepo kwenye mazoezi ya Manchester City siku ya Alhamisi. Mshambulizi huyo wa Norway amekuwa katika kiwango kizuri kwa City msimu huu, akifunga mabao 42 katika mechi 37 pekee tangu atue kutoka Borussia Dortmund


Hata hivyo ushiriki wake wikendi hii uko shakani kutokana na jeraha la kinena alilopata katika ushindi wa mabao 6-0 wa Kombe la FA dhidi ya Burnley.


Haaland hakusafiri kuungana na wachezaji wenzake wa kimataifa na Norway alipokuwa akiuguza jeraha lake kwa matumaini ya kuwa sawa kwa pambano kali na Liverpool Jumamosi 

Hata hivyo, kukiwa hakuna dalili zozote za mshambuliaji huyo katika mazoezi ya City, kunaweka uhusika wake katika mashaka makubwa.

Iwapo atakosa, ataungana na Phil Foden nje ya uwanja baada ya kiungo huyo wa kati wa Uingereza pia kuondolewa kwenye pambano hilo.

Ingawa hali halisi ya jeraha lake haijajulikana, baba yake, Alfie Haaland, alitoa taarifa kuhusu hali yake kwenye TV2 ya Norway ambayo inaweza kuwatia wasiwasi mashabiki wa City. 

Alfie Halaand alisema Man City inaweza kufanya kamali kumtumia katika mchezo dhidi ya Liverpool lakini ni wazi atahitaji matibabu maalum ili kuweza kushiriki mchezo huo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad