Muigizaji Irene Paul ametoa ya moyoni kwa kusema kuwa, wasanii wa Kibongo wasilaumiwe kwa kutoa filamu chini ya kiwango kwani zipo sababu zinazowalazimisha kufanya hivyo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Irene ameshusha waraka wake aliouita Rondom experience.
Wenzetu wakenya wamepiga hatua sana katika utayarishaji wa movie zao yani msanii anapewa script na malipo yake mavazi kuna stylist tayari kwa ajili ya kila msanii na uhusika wake.
Sisi watanzania ukipewa malipo mavazi utakayotumia ktk kazi ni juu yako (ndani ya labor charge) ndio maana mnaona nguo zile zile katika tamthilia tofauti ila sura ni moja,mavazi ya nyumbani na disco tunavaa ofisini etc.
Kwa style hii hata kuwa creative tunashindwa maana mtu unawaza script na nguo unayovaa,bado nywele (unajiamulia wigi moja mwanzo mwisho).
WHO CARES??Yes!! Maana hela tunapangia majukumu mengine kifamilia na ukikataa kazi anapewa mwingine unajionea sawa tu.
Kama tunataka ubora basi tuangalie hata huku,let's grow in all angles msanii abaki kama talent itasaidia kukuza na kutoa ajira kwa watu wenye uwezo wa kazi zao just saying.
Anyways msiwe mnalaumu wasanii kila kitu jamani,ITS NOT EASY FOR US EITHER."