Moja ya vitu vilivyo nichekesha hapo jana March 27, ni namna mashabiki wa Diamond walivyo ipokea playlist ya Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris kwa shingo upande, huku wengine wakitaka makamu huyo kuacha kiki anapo tembelea nchi za Afrika.
Wakati huu ambao Makamu wa Rais nchini Marekani, Kamala Harris yupo kwenye dhihara yake ya kisiasa barani Afrika huku akitarajiwa kuitembelea Tanzania ifikapo siku ya kesho Jumatano ya Machi 29,2023, Ametoa Playlist yake ya nyimbo za wanamuziki wa Afrika anazo zisikiliza sana katika mtandao wa Spotify kwa sasa hasa kwenye nchi anazo zitembelea ikiwemo Tanzania.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Flava waliomo kwenye Playlist hiyo ni Alikiba, Harmonize, Marioo, Platform, Abbah, Zuchu n.k. Kitu kilicho wachanganya mashabiki wa WCB, ni kutoona jina la Diamond kwa kuzingatia ukubwa wa jina lake ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Tuna ushabiki maandazi sana wa kulazimisha kila mtu awe shabiki wa tunao washabikia, Muziki ni ladha, na kila mtu ana muziki wake anaoweza u-feel anapo usikiliza, nilishawahi sema kama muziki usingekuwa una matabaka, tuna wasanii wengi wapya wenye vipaji vikubwa, nyimbo zao nzuri ila hazijafanikiwa kuwa Hits ila tunateswa na majina yaliyopo pale juu.
Kama sio matumizi mabaya ya mitandao, au matatizo ya akili ni nini?, Hivi kweli Kamala atafute kiki ya kuzungumziwa nchini kwa kuto orodhesha wimbo wa Diamond kimakusudi? Hivi hii nchi ina watu wa aina gani? Diamond ni nani apendwe na kila mtu, ukieleza kinyume na matarajio yao basi wewe una chuki, hivi tuko normal kweli au akili hazijafanyiwa subscription?
ELIMIKENI!📚