“Jambo la uchaguzi wa wachezaji kwa ajili ya timu ya Taifa ni la mwalimu, niwahakikishie watanzania Mwalimu alipewa 100% ya kuchagua wachezaji wa kikosi cha timu ya Taifa.”
“Kupitia mitandao nilikuwa naona watu wanalalamika mbona timu inachelewa kutangazwa, mwalimu alikuwa anafanya kazi pamoja na wasaidizi wake lakini alikuwa anajipa nafasi ya kuangalia mechi nyingine.”
“Kwa hiyo wachezaji wote waliokuwepo kwenye timu ya Taifa iliyopita na hii iliyopo, mwalimu alipata nafasi ya kuwaona wote!
“Kuchaguliwa timu ya Taifa kunategemea vitu vingi, wakati mwingine mchezaji anaweza kuwa mzuri lakini haingii kwenye mfumo wa mwalimu anaoutumia. Wakati mwingine mchezaji anaweza kuachwa ali arekebishe baadhi ya makosa, ni njia mojawapo ya kum-motivate mchezaji.”
“Lakini kwangu timu ya Taifa ni ya wachezaji wote, mchezaji akifanya vizuri kwa wakati husika kuitumikia timu ya Taifa ni kipaumbele.”
Mimi kwa sababu ni Kocha siku zote nampa mwalimu nafasi kubwa ya kufanya kazi yake kwa sababu yeye ndio anatakiwa afanye mazoezi na wachezaji na kutupa matokeo.”
“Kwenye mkataba kuna vitu ambavyo tumekubaliana kuvitekeleza, kwa hiyo mtu yeyote anaetaka kumuingilia mwalimu kwa namna moja au nyingine ni nani atawajibika?
“Sisi viongozi kazi yetu ni kutelekeza yale ambayo mwalimu anayataka ili aweze kufanya vizuri na ndio kitu ambacho tumekuwa tunakifanya siku zote.”
“Mimi niliwahi kuwa kocha, nilikuwa sitaki kuingiliwa kwenye mambo ya kiufundi, sasa hivi ni kiongozi siwezi kumuingilia kocha.”
- Wilfred Kidao, Katibu Mkuu TFF via @cloudsfmtz