Kosa la Ushoga au Usagaji UGANDA Miaka Kumi Jela



Bunge la Uganda jana Jumanne March 21,2023 limepitisha muswada wa sheria wa kupinga vitendo vya kufanya mapenzi ya jinsia moja ambapo kama Rais Museveni atausaini kuwa sheria Mtu yoyote anayehusika na vitendo vya kufanya mapenzi ya jinsia moja au yeyote atakayejitambulisha hadharani kama Mwanachama wa kundi la LGBTQ anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 jela.


Sheria hiyo inapendekeza hatua mpya kali zichukuliwe kwa Watu wanaojihusisha na mahusiano ya aina hiyo nchini Uganda ambako ushoga ni kitendo kisichokubalika.


Chini ya sheria inayopendekezwa, Marafiki, Familia na Wanajamii watakuwa na wajibu wa kuripoti Watu walio katika mahusiano ya jinsia moja kwa Mamlaka mbalimbali za kisheria.


Vitendo vya wapenzi wa jinsia moja tayari ni haramu Uganda, Wabunge wa Upinzani walilitaka Bunge kutoidhinisha muswada huo lakini Spika wa Bunge Anita Among amesema maadili na utamaduni wa Nchi hiyo lazima ulindwe.


Shirika la kutetea haki la Human Rights Watch linasema endapo sheria hiyo itaidhinishwa na Rais Yoweri Museveni, sheria hiyo mpya itakuwa ya kwanza mahali popote duniani kuharamisha Watu kujitambulisha kama Wapenzi wa jinsia moja, Watu waliobadili jinsia au Watu wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile yao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad