Kukiwa Bado Kuna Giza Totoro Fei Toto Aitwa Timu ya Taifa Stars




Kiungo wa Kimataifa wa Tanzania ambaye yupo kwenye mgogoro na Klabu ya Yanga SC, Feisal Salum Abdallah (Feitoto) amejumuishwa kwenye Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kitakachocheza michezo miwili ya kuwania kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Uganda (The Cranes).

Feisal amejumuishwa kwenye Kikosi hicho cha Kocha mpya wa timu hiyo, Adel Amrouche ambacho kina jumla ya Wachezaji 31 ambao mwezi huu (Machi 24 na 28, 2023) watapepetana na dhidi ya Uganda kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kufuzu AFCON nchini Ivory Coast.

Hata hivyo, Kocha Adel Amrouche amewajumuisha Wachezaji wengine ambao ni maingizo mapya katika Kikosi chake yupo, Ramadhan Makame (Bondrumspor - Uturuki), Yusuph Kagoma (Singida Big Stars), Ibrahim Baka (Yanga SC), David Luhende, Datius Peter na Abdallah Mfuko (Kagera Sugar).

Wengine ni Khalid Habibu (KMKM - Zanzibar), Alphonce Mabula (FK Spartak Subotica - Serbia), Edmund John (Geita Gold FC), na Yahya Mbegu (Ihefu SC).

Said Khamis (Al Fujairah - UAE), Himid Mao Mkami (Ghazi El Mahalla SC - Misri), Ally Msengi ( Swallows - Afrika Kusini), Haji Mnonga (Andershot Town - Uingereza), Ben Starkie (Basford United FC - Uingereza), Kelvin John, Mbwana Samatta (KRC Genk - Ubelgiji), na Novatus Dismas (Zulte Waregen - Ubelgiji).

Simon Msuva (Al Qadsiah - Saudi Arabia), Anuary Jabir (Kagera Sugar), Abdul Suleiman Sopu, Sospeter Bajana (Azam FC), Mudathir Yahya, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Kibwana Shomari, Metacha Mnata (Yanga SC), Beno Kakolanya na Aishi Manula (Simba SC).






Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad