Kumekucha Huko, Unaambiwa ili Fei toto Aachiwe Kuondoka Yanga Italazimika Kulipa Milioni 400, Patamu Hapo


Wakati vigogo waliowahi kuongoza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakifichua kwamba sakata la kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ linacheleweshwa na mchezaji mwenyewe na wao hawawezi kulimaliza bila kuwepo kwa mazungumzo ya mchezaji na klabu yake, wameeleza kama Yanga italazimika kumuuza, basi dau lake halitazidi Sh400 Milioni.


Feisal na Yanga waliingia kwenye mgogoro wa kimkataba, uliopelekea klabu hiyo kupeleka shauri kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF iliyomrejesha kiungo huyo Yanga.


Klabu hiyo juzi pamoja na mambo mengine, ilieleza iko tayari kumruhusu Feisal kuondoka kwa kuzingatia sheria za uhamisho zinazotambuliwa na TFF na FIFA na ikiwa kuna klabu inamhitaji, Yanga iko tayari kufanya mazungumzo wakati wowote.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad