Kwa Mayele Yanga Wamepata Mtu Sahihi Kukata Kiu yao ya Muda Mrefu


Mtazamo wa @kenny_mchambuzii

Nawarudisha nyuma kidogo ikiwa leo ni Throwback Thursday, Klabu ya Yanga ilifanikiwa kumtanbulisha mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele kuwa mchezaji wake mpya.

Katika msimu wake wa kwanza tu ndani ya Yanga Sc katika ligi kuu alifunga magoli 16 na kuwa namba mbili huku kiatu cha mfungaji bora ikichukuliwa na George Mpole.

Msimu huu unavyoanza hakuanza kwa kufunga sana, hii inachangiwa na uchovu kwa kiasi kikubwa kutokana na kutumika sana msimu uliopita na kuisadia Yanga Sc kubeba Ubingwa wa Ngao ya Jamii,Ligi Kuu na Fa.

Gari lilivyoshika moto kwa Mshambuliaji mambo yakabadilika ghafla na kuanza kufunga na kuwa katika kiwango bora sana.

Fiston Kalala Mayele kwa sasa ndio Mshambuliaji wa mfano katika Ligi yetu, Umbo lake,anajua kukaa kwenye nafasi,ni ngumu kumnyang'anya mpira na ana jicho la kuona goli la wapinzani wake.

Mpaka sasa katika Ligi Kuu ya NBC kwa msimu huu tayari ana magoli 15 huku anayemfatia (Saido na Phiri) wakiwa na magoli 10 kila mmoja.

Wakati Mwamba wa Umalila @baraka_mpenja akimpa Fiston Mayele jina la (KING) Mayele hakika Ufalme wa Mayele unaonekana.

Jicho la @caamil_88 na jopo la SCOUTS waliohusika kumleta FISTON MAYELE Yanga Sc kwa hakika wameonyesha ukubwa wa Yanga Sc na sasa Wananchi wanafurahi.

Kipindi cha nyuma Yanga Sc walikua na Washambuliaji lakini viwango vyao havikuridhisha na ngumu kumaliza Ligi wakiwa na magoli 15+ lakini kwa sasa wamepata mtu haswa na aliyekata kiu yao kwa muda mfupi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad