Luteni Kanali Gaudentius "Epukeni Matapeli Nafasi za Kazi JWTZ Haziuzwi"



 Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema katika nafasi zilizotangazwa leo za Vijana wa JKT kujiunga katika Jeshi hilo, wapo Matapeli watakaojitokeza ili kuwaibia Watu fedha kwa madai ya kuwauzia nafasi ambapo limesema nafasi hizo haziuzwi.


Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda akiwa Dodoma leo amesema “Natambua katika matangazo haya ya kujiungana Jeshi kuna mwanya wa Matapeli utaibuka, Matapeli watapenda kutumia fursa hii, niwaombe Watanzania wote, Vijana na Wazazi wetu wasikubali Mtu kumwambia ‘nipigie simu kwamba nina fomu ya kujiunga’ kwanza hatutoi fomu”


“Mtu atakuambia ‘nina nafasi ya Kijana wako uliyoniomba sasa nafasi imepatikana, nina Afande ninamfahamu yupo Makao Makuu ya Jeshi ana nafasi zake nipe hela nikufikishe kwake’, ndio maana Afande mwenye nafasi hizo Jeshini hayupo nafasi zipo kwa haki sawa tutawapima kwa vigezo vyao”,


“Watanzania wasikubali kudanganyika hakuna njia ya mkato kwenye kupata hizi nafasi, katika hili la kupigiwa simu najua kwenye msafara wa mamba na kenge wapo kuna utapeli utaibuka, msikubali kutapeliwa”

BONYEZA HAPA KUSOMA  NA KUAPPLY NAFASI ZA AJIRA JWTZ ZILIZOTANGAZWA LEO

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad