Mabosi Yanga Watoa Kauli Ya Kutisha Kombe la Shirikisho






WAKATI jana wakicheza mechi yao ya tano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir ya Tunisia, uongozi wa Yanga umebainisha wazi kuwa bado wataendelea kuishi na ndoto yao ya kubeba ubingwa wa Afrika hata kama wakiukosa msimu huu.

Yanga kwa msimu huu wapo kwenye nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo hadi jana walikuwa wanashikilia nafasi ya pili kwenye Kundi D wakiwa na pointi saba.

Katika mchezo huo wa jana Yanga walikuwa wanahitaji ushindi kwa ajili ya kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua inayofuata kabla ya kwenda ugenini nchini DR Congo kucheza na TP Mazembe kwenye mchezo wao wa mwisho.


Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji
Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji ameliambia Championi Jumatatu, kuwa wao wataendelea kuwa na ndoto hiyo ya kuwa timu ya kwanza ambayo italeta taji la Afrika nchini.

“Malengo yetu sisi kama viongozi ni kuhakikisha kuwa tunafanikiwa kuuleta ubingwa wa michuano ya kimataifa hapa nchini na kuwa timu ya kwanza kufanya hivyo kwa timu kutoka katika taifa hili.

“Hata kama sio msimu huu lakini itakuwa kwa misimu mingine, Yanga tunayo nia hiyo ya kuhakikisha kuwa tunafikia malengo yetu na tunaamini kuwa inawezekana, kikubwa ni mashabiki kuwa na sisi bega kwa bega,” alisema kiongozi huyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad