Maneno Aliyotoa Costa Titch Wakati wa Kifo cha AKA "Tumeshindwa Mtihani wa Kujua Tutaondoka Muda Gani"


“Bado sihisi kama ni kweli.... Nitakupenda siku zote kaka” ni maneno ambayo Rapa tokea South Africa , @costatitch aliyachapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, February 13 siku 3 baada ya kifo cha Rapa wa South Africa pia @akaworldwide

Ikiwa maneno hayo hayajatimiza hata mwezi tangu Titch ayaandike kama sehemu ya kuomboleza kifo cha AKA, Hit maker huyo wa SUPERSTAR ambaye amefanya kazi nyingi na wasanii wa Bongo Flava hasa tokea WCB, amefariki dunia pia.

Ni safari ya Rappers wawili iliyotenganishwa na siku kadhaa tu. Ni mtihani ambao binadamu tumeshindwa kuufaulu, kujua dakika zijazo nini kitatokea kwenye maisha yako, iwe kizuri au kibaya.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad