Marufuku Yapigwa Kupost Watoto Wadogo Mitandaoni


Wazazi Nchini Ufaransa wanaweza kupigwa marufuku ku-post picha za Watoto wao kwenye mitandao ya kijamii iwapo mswada mpya uliowasilishwa wiki hii utapitishwa kuwa sheria.


Mswada huo utaipa Mahakama mamlaka ya kuwapiga marufuku Wazazi kuweka picha za Watoto wao mtandaoni ambapo wote wawili watawajibikia katika kusimamia haki za picha za Watoto wao huku uamuzi wowote wa kuzipost mtandaoni ukitakiwa kuzingatia umri wa Mtoto pamoja na kiwango cha ukomavu wake.


Sheria inayopendekezwa inakuja baada ya muamko wa wazazi wengi kupost picha za watoto wao mitandaoni jambo ambalo huitwa “sharenting” ikijumuisha moja ya jambo kuu linalo hatarisha haki za faragha za watoto, kulingana na taarifa ya maelezo ya mswada huo pia ilisema asilimia 50 ya picha zinazotumiwa kwenye majukwaa ya ponografia ya watoto hapo awali zilichukuliwa kupitia picha zilizopostiwa na wazazi wenyewe kwenye mitandao ya kijamii.


Kwa mujibu wa Daily Mail, mswada huo bado unahitaji kupitishwa katika Bunge la Seneti ya Ufaransa kabla ya kusainiwa na kutangazwa na Rais kuwa sheria

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad