UONGOZI wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema watumiaji wa mfuko huo waliomo kwenye kundi la watoto, wakiwamo wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na elimu ya juu, ambao walikuwa kwenye kifurushi maalum kwa kulipia Sh. 50,400 kwa mwaka, sasa hawatatumia utaratibu huo.
Mfuko huo sasa una utaratibu mpya ulioanza jana Machi 13, kundi hilo linalazimika kulipiwa malipo yao kupitia uanachama wa wazazi au walezi wao ambao ni wanachama kupitia vifurushi vya mfuko kulingana na ukubwa wa familia.
Vifurushi hivyo ni vilivyopewa majina ya Najali Afya, Timiza Afya na Wekeza Afya.
Januari mwaka huu, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, alisema atasimama kidete kuhakikisha kila Mtanzania anafahamu umuhimu wa kuwekeza na kuweka kipaumbele kwenye afya na hakutakuwa na msamaha wowote.
Waziri Ummy alisema ajenda kuu iliyopo mbele ya sekta hiyo ni huduma bora na Bima ya Afya kwa Wote, ambayo kwa sasa kiwango kinachotazamiwa ni kuwa kati ya Sh. 340,000 hadi 360,000 kwa mwaka, ili kuhudumia watu sita kwa huduma za rufani, kanda na kibingwa.
UTARATIBU MPYA
Meneja Uhusiano wa NHIF, Angela Mziray, jana aliiambia Nipashe iliyotaka kufahamu utaratibu mpya kuhusu huduma hizo, kwamba utaratibu huo ulianza rasmi jana na bei za vifurushi kulingana na familia wachangiaji kuanzia umri wa miaka 18 hadi 35, ni kuanzia Sh. 192,000 kwa huduma za kifurushi cha Najali Afya; Sh. 384,000 (Wekeza Afya) na Sh. 516,000 kwa Timiza Afya.
Aidha, kifurushi kama hicho yaani mtu mmoja, bila wategemezi, kwa wachangiaji kuanzia umri wa miaka 35 hadi 59 gharama ni Sh. 240,000 kwa huduma za kifurushi cha Najali Afya; Sh. 444,000 (Wekeza Afya) na Sh. 612,000 kwa Timiza Afya.
Kadhalika, vifurushi kwa ajili ya wanandoa pamoja na mtoto mmoja kwa wachangiaji kuanzia umri wa miaka 18 hadi 35, ni Sh. 504,000 kwa kifurushi cha Najali Afya; Sh. 924,000 (Wekeza Afya) na Sh. 1,272,000 kwa kifurushi cha Timiza Afya.
Pia kifurushi kwa ajili ya wachangiaji kuanzia umri wa miaka 36 hadi 59 wakijumuishwa watoto wawili, gharama ni Sh. 696,000 (Najali Afya); Sh. 1,248,000 (Wekeza Afya); Sh. 1,728,000 (Timiza Afya) kwa mwaka.
"Ni kweli kuna utaratibu mpya na maboresho kuhusu usajili wa watoto. Watoto walikuwa wanaweza wakaingia kama watoto wenyewe, maboresho yaliyofanywa sasa hivi, wanahitaji watu waingie kama familia, kaya au kupitia shule zao.
"Sio awali ilikuwa mtoto mmoja, ilikuwa na changamoto na malalamiko mengi ikiwamo kupita miezi mitatu ili uanze kuhudumiwa, utakuta mtoto anakuja anasajiliwa, lakini mzazi wake sio mwanachama, au utaratibu wa kishule, waingie kama shule," alisema.
Angela alisema utaratibu huo unawagusa wanachama wa mfuko huo ambao malipo yao yamefikia kikomo na kwamba wakitaka ku-renew (kupitia) bima hizo, wajiunge kupitia utaratibu wa familia, kaya au wazazi wao ambao wanahudumiwa na kampuni au taasisi fulani.
"Sasa hawa watasajiliwa kama kaya, makundi au shule zao. Msingi, sekondari kama ilivyokuwa kwa vyuo huja kama chuo wakiwasajili. Utakuta mzazi hana bima, ila anasubiri mtoto akiumwa ndipo amsajili mtoto wake, hii ni risk (hatari)," alisema Angela.
Kwa utaratibu huo, Angela alisema matarajio ni kundi kubwa la watu kujisajili kupitia vifurushi na kwa kipindi cha mwezi mmoja, waliojiunga kama shule, familia au vikundi watakuwa wanaanza kuhudumiwa na mfuko huo tofauti na awali, ikiwapasa kusubiri miezi mitatu.
"Vifurushi mama anaweza akaingia na mtoto mmoja, au baba na watoto wawili. Kujisajili sasa itabidi shule zisajili watoto wao, wazazi waamue utaratibu huu na shule wajiunge na kuwa na kundi la wanafunzi. Usajili utapitia shule, ingawa tutaangalia baadaye kama utasuasua," aliongeza.
Angela alisema kwa wanachama wa vikundi ikiwamo vya umoja wa tasnia tofauti, ikiwamo waandishi wa habari, ambao kila mwanachama alilipia Sh. 100,000 kwa mwaka, mazungumzo yanaendelea na iwapo kutafanyika maboresho, yatawekwa hadharani.
MAONI WANACHAMA
Baadhi ya wazazi, walezi na watumiaji wa huduma za NHIF, wakizungumza na Nipashe jana, walisema hatua ya serikali kusitisha utaratibu wa kulipia upya (renew) bima za watoto waliopo, uangaliwe kwa umakini kwa kuwa unaweza kusababisha mtoto kukosa huduma ya matibabu kutokana na kukosa fedha taslimu ya kulipia.
Denis Brighton alisema ni kawaida kufanya malipo ya bima ya afya ya mwanawe kila mwaka, akisema kila mwaka huduma hiyo inapokaribia kufikia ukomo hupewa taarifa na mfuko huo ya kutakiwa kulipia.
“Nimetumiwa taarifa na NHIF na ujumbe ni huu mwandishi, unanieleza nifike ofisi za bima ya afya ku-renew (kuhuisha) uanachama kwa kulipia Sh. 50,400 kwa ajili ya bima ya mtoto wangu, ninafika hapa ninaambiwa siwezi ku-renew, unakuja utaratibu mpya.
“Kinachonishtua bima hii ni ya mtoto. Je, akiumwa inakuwaje? Wakanijibu nitalipia fedha cash (taslimu). Kadi ya bima ya mtoto wangu inaonyesha inatumika miaka mitano, yaani itaisha mwaka 2026 na kwa mfumo wa kulipia kila mwaka," alisema Denis.
Agnes Magwa alisema utaratibu huo unaweza kuwa mzuri ingawa kwa sasa tatizo lipo katika maandalizi, ili mzazi kumudu gharama ya vifushi hivyo kwa mwaka.
“Ilikuwa Sh. 50,400 tu ninamlipia mtoto mmoja, nilimudu kila mwaka, nilikuwa nipo radhi mimi nisijilipie huduma ya mfuko, ila angalau niwe na uhakika wa mtoto wangu kutibiwa," alisema Agnes.
WAZIRI
Waziri wa Afya, Ummy, akizungumza hivi karibuni, alisema mfuko huo unaelemewa kutokana na kulipia gharama kubwa kwa ajili ya magonjwa yasiyoambukiza (NCD), miongoni mwake ni kisukari, kiharusi na shinikizo la juu la damu, ikifahamika zaidi kwa jina la presha.
Alisema magonjwa hayo yameugharimu mfuko takribani Sh. billioni 99.09 kwa kipindi cha mwaka 2021/22 na hali hiyo inahatarisha mfuko, akisema njia pekee kwa jamii ni kupatiwa elimu kuepukana na magonjwa hayo.
Alibainisha NHIF inatoa huduma kwa wanachama milioni 4.33, sawa na asilimia nane ya Watanzania wote wapatao milioni 60, huku asilimia sita wakihudumiwa na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
40
habarileo.co.tz
Wema Sepetu atambulishwa ukweni! “Mimi nikipenda, nimependa”
21
bongo5.com
Habari mpya
Kasi ndoa za jinsia moja ni kuiandaa dunia kuwa ‘jangwa’
3h
ippmedia.com
MO Dewji: Nimemsamehe Haji Manara
2
9h
dar24.com
CHADEMA, ACT watoa ya moyoni
4h
ippmedia.com
Young Africans: Tunamtaka yoyote Kombe la Shirikisho
2h
dar24.com
Work a USA Job From Home in Tanzania, United Republic Of. Salaries May Surprise You
USA Jobs from Home | Search Ads
Unsold Laptops May Be Sold for Nothing (Take a Look at the Prices)
Unsold Laptop Deals
by TaboolaSponsored Links
86
59
189
Tujadili swala hili
Unmute
Unmute
Asante sana kwa Taarifa hiz Muhimu sana kwa JAMII ZETU na afya ya Umma Kwa ujumla.
ReplyDelete