Mayele, Musonda Waipa Jeuri Yanga Kuvaana Na Geita Gold Uwanja Wa Azam Complex Leo

 


KIWANGO bora kinachoendelea kuoneshwa na Yanga katika mashindano mbalimbali msimu huu, kimemuibua Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said ambaye ameweka wazi kuwa, wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri na kuandika historia mpya katika Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.


Yanga ambao leo Jumapili wanatarajiwa kushuka kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar, kuvaana na Geita Gold katika mchezo wa wa Ligi Kuu Bara, ndio wawakilishi pekee wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa Kundi D.


Yanga wamekuwa kwenye kiwango bora msimu huu ambapo baadhi ya mastaa wa kikosi hicho akiwemo Fiston Mayele na Kennedy Musonda, wakionesha uwezo mkubwa katika mashindano tofauti.


Kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi, Mayele na Musonda wamechangia mabao matatu mpaka sasa.


Akizungumza na Spoti Xtra, Injinia Hersi alisema: “Tunafurahia ubora wa kikosi chetu na matokeo ambayo tumeendelea kuyapata, hii inaonesha ni kwa kiasi gani kama timu tumeamua kufanya makubwa msimu huu.


“Kwenye Kombe la Shirikisho Afrika tuna nafasi nzuri ya kucheza robo fainali ikiwa tutaibuka na ushindi dhidi ya US Monastir, tunaamini kuwa kwa ubora wa kikosi tulionao tunaweza kuandika rekodi katika mashindano ya Afrika msimu huu.”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad