Katika ukurasa wake wa Instagram wenye wafuasi zaidi ya laki mbili, imetoka taarifa kuthibitisha kifo cha mchekeshaji kutokea Ghana, @ahoufe__official aliyejipatia umaarufu zaidi kwenye mitandao ya Tiktok na Instagram kutokana na muonekano wake kufananishwa na 2pac.
Ahoufe aliuvaa uhusika wa 2pac kwa kiasi fulani ikiwemo kujifunga Bandana kichwani kama 2pac na mitoko ya Old School ambayo ilikuwa ikitupiwa na legend huyo kwenye Hip Hop duniani.
Maradhi yaliyo ondoa uhai wake hayajawekwa wazi lakini post iliyotoa taarifa za kifo chake, imeweka wazi jamaa alikuwa akiugua kwa muda mrefu licha ya kuendelea kuwafurahisha watu mitandaoni. Inadaiwa amefariki siku ya jana tarehe 29 March.
R.I.P 2pac of Africa.