Polisi nchini Afrika Kusini wanamtafuta mfungwa aliyeghushi kifo chake na kutoroka gerezani na kuingia mitandao ya kijamii akiendelea ‘kuchati’ na wasichana wanaomfahamu.
Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Tuko’ wameeleza kwamba idara za usalama zilikuwa zimeamini kuwa Thabo Bester amefariki dunia baada ya kujichoma moto katika Gereza la Bloemfontein Mei 2022.
Hata hivyo, polisi waligundua Jumapili, Machi 26, kupitia vipimo vya DNA kuwa mabaki yaliyopatikana kwenye seli ya mtu aliyejichoma moto gerezani yalikuwa ya mtu mwingine.
Polisi wameeleza kwamba uchunguzi wa maiti ulibaini kuwa mtu aliyepatikana akiwa amefariki hakuwa mfungwa wa ubakaji.
"Kwa wakati huu tunaendelea kumtafuta mfungwa huyo na kufuatilia jinsi alivyoghushi kifo chake," Msemaji wa Polisi, Athlenda Mathe amesema hayo.
Awali, Bester anadaiwa kuwahadaa waathiriwa kwenye mtandao wa kijamii kabla ya kuwabaka na kuwaibia huku mmoja wa waathiriwa akiuawa.
Mwaka 2012, Bester alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani akipatikana na hatia ya ubakaji, wizi na mauaji.
Mashaka kuhusu kifo cha Bester yaliibuliwa kwa mara ya kwanza na kituo cha habari cha Ground Novemba mwaka jana.
Picha zinazodaiwa kumuonyesha mfungwa huyo akinunua vitu jijini Johannesburg ziliambaa mitandaoni.
Wakati huohuo baadhi ya wanawake wamejitokeza wakidai mhalifu huyo aliwasiliana nao kwenye mitandao ya kijamii kwa mara nyingine.
Mashaka kuhusu kifo cha Bester yaliibuliwa kwa mara ya kwanza na kituo cha habari cha GroundUp Novemba mwaka jana.
Picha zinazodaiwa kumuonyesha mfungwa huyo akinunua vitu jijini Johannesburg zilionekana mitandaoni.