Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) CPA Charles Kichere lwo Ikulu akiisoma ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2021/2022, amesema deni la Serikali kwa sasa ni Tsh. Trilioni 71.31.
“Deni la Serikali kufikia June 30,2022 lilikuwa Tsh. Trilioni 71.31 ikilinganishwa na Tsh. Trilioni 64.52 lililoripotiwa kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kuna ongezeko la Trilioni 6.79 sawa na 10.5%, ambapo kipimo cha deni la Serikali kinachotumia pato la Taifa kinaonesha Deni hili ni himilivu”
Akiongea kuhusu deni hilo la Taifa baada ya CAG kumaliza kusoma Ripoti hiyo, Rais Samia amesema yafuatayo ——— > “Mwenendo wa Deni la Serikali tunakopa ndio, tunakopa kwa maendeleo lakini tunakopa kwa akili, tusipokopa hatutofanya maendeleo lakini lazima tukope mikopo yenye unafuu tufanye maendeleo”
“Tuko vizuri, mikopo ndio maendeleo tutaendelea kukopa lakini tuko makini kwamba lazima tuwe chini ya viwango tulivyowekewa” ——— Rais Samia.