Mrembo Black Chayn Aokoka, Aamua Kuondoa Makalio ya Bandia


Mwaka mmoja baada ya mwanamitindo na aliyekuwa wifi wa Kim Kardashian, Blac Chyna kuokoka, amefikia uamuzi wa kuachana na baadhi ya mambo aliyopenda kuyafanya.

Blac Chyna ameondoa mchoro unaodaiwa kuwa wa kishetani aliokuwa amejichora 'Baphomet tatoo', pamoja na kuondoa vile alivyojaza usoni ili kubadili mwonekano wake (lip fillers na face fillers).

Pia ameondoa makalio bandia ambayo yalikuwa sehemu ya utambulisho wake kwa kipindi kirefu.

Kwenye ukurasa wake wa......Blac Chyna amesema "Wote mnajua kuwa nina 'tattoo' ya Baphomet, sawa, lazima itoke. Ninakaribia kutokuwa na alama ya mnyama mwilini mwangu." amesema Chyna na kuongeza kusema kuwa
"Lakini nitakuambia hivi, nilipoichora tattoo mara ya kwanza, hiyo haikuwa maana yake na bila kujali sitaki kitu chochote hasi au cha kishetani kwenye mwili wangu tena."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad