Msanii Roma Afunguka "Wasanii Msidharau Kazi za Wasanii Wenzenu"

 


Roma Zimbabwe anakerwa na tabia za baadhi ya wasanii kudharau kazi za wengine.


Ametumia Twitter kuelezea suala akisema, “Ewe msanii kama unataka kutoa wimbo wako wewe toa tu na upromote kimpango wako pasi ku-underrate efforts za wasanii wenzako.


Hii tabia unatoa wimbo then ukihojiwa unasema, ‘ujue game hapa katikati ilikuwa kama imelala hivi so nimeona nije kuichangamsha.’


Sikia mwanangu, game haijawahi kulala hata siku moja. Madogo wanapiga kazi na wanakichafua haswaa kama huwaoni sisi tunawaona. Unamskia msanii anasema, ‘unajua hip hop ililala saaana hapa katikati, nimekuja sasa kuiamsha.’


Weee bwana hebu usitukwaze, tena hapo kwenye Hip-Hop ndio usipaguse kabisaaaaa tutagombana sana. Hip-hop haijawahi na haiwezi kulala….milele yote!!


Nimeandika kwa hisia kali sana na uchungu mithili ya #msimbe aliyenyimwa urithi.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad