Meneja uhusiano @taasisiyamifupa_moi Patrick Mvungi amesema “Milanzi alipokelewa MOI tarehe 22/2/2023 ambapo alipata huduma za kibingwa katika kitengo cha dharura (EMD), ICU, HDU na wodi 2A “
“Milanzi alipokelewa MOI akiwa ameumia maeneo ya kichwa, mguu wa kushoto, mkono na bega upande wa kulia ambapo ataendelea na huduma kama Mgonjwa wa nje na atarudi kliniki baada ya wiki mbili”
“Tunatoa shukran za dhati kwa Watanzania wote, vyombo vya habari ambao kwa pamoja wameshirikiana nasi katika kumuombea na kumtangaza Osam Milanzi”