Kisa cha Simba Mtawala wa eneo la namiri katika Mbuga za Serengeti, Bob Jonior kinaendelea kwa kuchukua sura mpya baada ya wauaji saba kupachikwa jina la Seven Killers na mmoja wao anakuwa Mtawala na amemchukua simba jike mtoto wa Bob Jonior.
Kwa mujibu wa waongoza watalii wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti, inaelezwa kuwa Bob Junior akiwa na mwenzake walipewa taarifa kupitia miungurumo kuwa kuna simba wamevamia eneo hilo, simba mfalme huyo alikaidi na kwenda kupambania himaya yake huku mwenzake akikimbia kusikojulikana.
Inaelezwa pia kuwa si mara ya kwanza kwa Bob Junior kujaribiwa kupibduliwa, amara kadhaa imekuwa ikitokea lakini anashinda jambo ambalo safari hii imekuwa tofauti kwani limesababisha kugharimu uhai wake.
Kwa asili ya wanayama wanaoishi porini, hasa simba, ni marufuku kuingilia nature (asili) ya maisha kwa sababu ndivyo wanavyoishi. Tawala inapoikuwa lazima itokee tawala nyingine kuhitaji hiyo miliki na kuangamiza tawala nyingine iliyopo.
Bob Jr ndiye simba aliyepata miliki ya utawala bila kupindua utawala wowote, mara baada ya baba yake aliyekuwa akijulikana kama Bob Maley na mdogo wake aliyeitwa ZIggy kuuawa.
Kisa cha kuitwa Bob Maley kilitokana na nywele zake (manyoya ya kichwani na shingoni) kuwa mengi na kusokota kama rasta za mwimbaji wa zamani wa Reage, hayati Bob Maley kutoka Jamaica.
Baada ya kifo cha baba yake, Bob Junior akiwa na umri wa miaka miwili tu alikimbia akiwa mdogo mpaka sehemu inayoitwa Namiri.
Huko alikuta hakuna simba anayetawala eneo lile, hivyo aliamua kupiga kambi na kujimilikisha eneo hilo, miaka mingi mpaka alipopinduliwa hivi karibuni na simba wajulikanao kama seven brothers.
Baada ya kutawala eneo hilo kwa miaka mingi na kufanikiwa kupata kizazi kikubvwa, aliwatimua baadhi ya vijana wake kwenye himaya yake akiamini wamekuwa wanahitaji kwenda kujitegemea na kutafuta mawindo yao.
Mmoja wa wale simba saba walioshirikiana kumuua Bob Junior ambaye ndiye alionekana akimalizia kutekeleza mauaji hayo kwa kumvunja kiuno Bob Jr, simba huyo amepewa jina la Bob Killer ama King Killer na ameonekana kwenye himaya ya mfalme huyo akiwa na binti wa Bob Junior.
Simba huyo jike anatajwa kama kuwa ni moja ya kizazi cha Bob Junior. Ikumbukwe kuwa, Bob Jr ana jumla ya vizazi vine ambapo si kitu cha kawaida kwa simba. Kwa kawaida simba ana uwezo wa kuishi vizazi viwili tu ama kimoja, lakini bob Jr amekaa miaka 13 ndiyo maana amepata kizazi kingi kuliko kawaida.
Bob Killer na binti wa Bob Junior wameonekana kwenye tawala ya marehemu huyo hali inayoashiria kama wapo kwenye fungate na huenda ndiye akamuoa. Inasemekana kuwa kwa jamii za simba, siku za usoni anatarajiwa kumzalisha binti huyo.
Tayari fisi wameshashambulia mzoga wote wa Bob Junior na kumaliza kabisa mabaki ya mwili wa simba huyo.