Mwamba Ajifungia Ndani na Mkewe Kisha Kuunguza Nyumba na Moto



Hamis Pius (41) Mkazi wa Nyigamba Jijini Mbeya amefariki kwa kuungua moto baada ya kujifungia ndani ya chumba anacholala na Mkewe Rebelia Makoso (38) kisha kumwaga mafuta ya Petroli na kuwasha moto

Kelele za Rebelia zikasababisha Mtoto wake, Mkeshilisi Hamis (21) kwenda kutoa msaada na kumuokoa. Baba yake alikataa kutoka ndani na kuungua hadi kupoteza maisha

Kamanda wa Polisi Mkoa wa #Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga amesema uchunguzi wa awali umebaini chanzo ni wivu wa Mapenzi. Mke na Mtoto wa Marehemu wanaendelea kupatiwa matibabu Hospitali Teule ya Ifisi ya Mbalizi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad