Athari za kiuchumi za janga la UVIKO-19 na vita vya Urusi na Ukraine vimefanya iwe vigumu zaidi kwa nchi nyingi za Afrika kulipa madeni yao. Sasa, mataifa 22 ya Afrika yanakabiliwa na mzozo wa madeni au yako katika hatari kubwa ya kukumbwa nayo.
China ni mkopeshaji mkuu wa mataifa mengi ya Afrika, lakini mikopo yake imeshuka katika miaka ya hivi karibuni, hali inayotabiriwa kuwa mbaya kwa mwaka 2023 na kupunguza uwezo wa mataifa ya Afrika kupata fedha zinazohitajika ili kufanya uboreshaji wa kijamii kwa watu wao na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Mwaka 2020 mataifa saba ya Kiafrika yaliripotiwa na Benki ya Dunia kuwa katika matatizo ya kifedha au hatari ya kuelemewa na madeni kutokana na wingi wa ufadhili wa China.