Nicki Minaj Adai Kuna Watu Wanatumwa Wamtukane ili Aanguke Kimuziki


Nicki Minaj anakiri kuna harakati za watu kushuhudia anguko lake ambapo rappers wa kike wanalipwa ili kum-diss.

Nicki ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye utambulisho wa ngoma yake mpya ‘Red Ruby Da Sleeze.’

Pia amezungumzia uhalisia wa Hip Hop na hali ya wasanii wa sasa.

“Ukiandika na kurap, unakuwa bora kila siku, lakini nadhani kwa sababu ya upepo wa wasanii wa TikTok kupata deals, watu wa Instagram kupata likes halikadhalika na watu wa Twitter, labels za wasichana na management companies zimekuwa zikilipia viral tweets ambazo ni diss kwa Nicki Minaj,” amesema.

Nicki ambaye anazindua label yake mwenyewe na tayari ameshamsaini Nana Fofie wa Ghana, anaamini sio sawa kumfananisha yeye na watu wengine ambao hawaandiki mistari yao wenyewe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad