Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amefungua Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara Jijini Dodoma leo ambapo amewataka Viongozi kujiepusha na matumizi ya Walinzi binafsi na Waandishi wa Habari binafsi bila kufuata taratibu kwakuwa inahatarisha usalama wao binafsi na wa siri za Serikali.
“Naamini Watoa mada mtatoa msisitizo kuhusu matumizi ya Walinzi binafsi, wamekuwepo Watu wanajichukulia Walinzi binafsi (Body Guard) na Waandishi wa Habari binafsi katika Ofisi za Umma, sasa zipo taratibu za kufuata endapo itabainika Kiongozi anahitaji kupatiwa Wasaidizi wa aina hii kwahiyo zingatieni taratibu zilizopo na sio vinginevyo”
“Kiongozi asipofuata utaratibu unaotakiwa kuwapata Watumishi hawa na kuamua kujitafutia mwenyewe wakati mwingine inakuwa sio salama hata kwa Kiongozi mwenyewe na hata siri za Serikali”
“Kuweni makini na maneno mnayozungumza kupigapiga story na Wasaidizi wenu hususani Madereva wetu na Watu wengine mnapokuwa nje ya Ofisi zenu au hata sehemu za starehe ili kuepuka kutoa siri za Serikali”