Rais Samia: Acheni kauli ya 'Maelekezo kutoka juu

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akifunga Mkutano wa Faragha (Retreat) wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC) Jijini Arusha, leo tarehe 04 Machi, 2023.


RAIS SAMIA ANAZUNGUMZA Yapo mataifa ambayo yana watu wachache na ardhi yao ni ndogo lakini kwa kuwa uongozi wao ni bora yameendelea na furaha ndani ya Nchi ni kubwa, naamini sisi viongozi katika nafasi zetu tukibadilisha mitazamo yetu na kuacha mazoea tunaweza kuleta mafanikio makubwa.


Mitazamo yetu ikibadilika ni wazi migongano na mapambano sehemu ya kazi havitakuwepo, ubadhirifu utaisha, utendaji wa kazi utaimarika.


Niwasihi baada ya mafunzo haya twende tukaache migongano, kusengenyana, tukaaminiane, tuache uvivu, uzembe ili tukafanye kazi za watu kubwa zaidi tukaache dharau.


Tunawahudumia Wananchi wenye nchi, wala tusidharauliane wenyewe kwa wenyewe.


MAWASILIANO NDANI YA SERIKALI Twende ngazi kwa ngazi, kosa kubwa tunalofanya ndani ya Serikali ni kudhani mawasiliano yamefanyika, tunasahau taarifa na mawasiliano.


Taarifa ni pale unapolisema jambo lakini haina maana itafika kule unapokusudia, ili ifike lazima kuwe na mawasiliano, pia hakikisha jambo lako limefika usidhani.


JIAMINI Kama ukijiamini utafanikiwa, usipojiamini unajiwekea vikwazo mwenyewe, ukijiamini utapata mbinu, nendeni mkafanye kazi kwa kujiamini, aminini uwezo wenu, mnapofanya maamuzi sema haya ni maamuzi yangu.


Sema nimeamua haya kutoka na hali hii au hii, tusielekee kusema ‘haya ni maelekezo kutoka juu’, hiyo utakuwa haujiamini, fanya mamuzi kwa kujiamini na uwe tayari kutetea maamuzi yako.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad