Rais US Monastir aivulia kofia Young Africans



Rais wa Klabu ya US Monastir kutoka nchini Tunisia, Ahmed Belli, ameipongeza Young Africans kwa kufuzu hatua ya Robo Fainali kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Juzi Jumapili (Machi 18), Young Africans ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya US Monastir kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, na kufuzu hatua ya Robo Fainali.

Belli amesema: “Tumepoteza mchezo wetu mbele ya Young Africans, yote haya ni matokeo ya mpira wa miguu, tunachoangalia sasa ni namna gani tutakavyojiandaa kwa ajili ya mechi za hatua ya Robo Fainali.

“Nawapongeza sana Young Africans kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza katika michuano hii, nawatakia kila la kheri kwenye hatua ya robo fainali na naamini watafanya vizuri zaidi ya walivyofanya katika hatua ya makundi.”


Kwa sasa Young Africans inaongoza Kundi D na inaweza kukutana na Marumo Gallants (Afrika Kusini), USM Alger (Algeria), Saint-Éloi Lupopo (DR Congo) au Al Akhdar (Libya) zilizopo Kundi A, za Kundi B ni Rivers United (Nigeria) na ASEC Mimosas (Ivory Coast) au zile za Kundi Kundi C, ASFAR (Morocco), Pyramids na Future (Misri).
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad