Ripoti ya pili ya uchunguzi wa ajali ya ndege ya Precision Air Yazua Mengine


Ripoti ya pili ya uchunguzi wa ajali ya ndege ya Precision Air iliyoanguka Ziwa Victoria mkoani Kagera na kuua watu 19 ambayo imetolewa na Taasisi ya Uchunguzi wa Ajali za Ndege (AAIB) chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeeleza kuwa waongozaji wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza waliwajulisha marubani wa ndege hiyo na kuwashauri kwenda kutua Mwanza lakini wao waliamua kutua Bukoba.

Mkurugenzi Msaidizi wa Uchunguzi wa Ajali za Ndege, Redemptus Bugumola amesema ripoti hiyo ni tofauti na ripoti iliyotolewa Novemba 23 mwaka jana ambapo amebainisha kuwa uchunguzi umefanyika kwa kina ukijumuisha vinasa sauti vilivyokuwa katika ndege hiyo.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa wakati ndege ikikaribia kutua Bukoba ilisikika sauti (alarm) mara tatu ikiwaonya marubani kuwa wako karibu kugusa ardhi lakini wachunguzi wanasema marubani hawakufanya lolote, huku sauti za majadiliano ndani ya chumba cha marubani zilirekodiwa ambapo rubani msaidizi alisikika akipaza sauti mara mbili ya kumtaka rubani mkuu kuacha kutua na airushe ndege juu lakini hakujibiwa.

Aidha, ripoti imedai aliyehusika kufungua mlango wa ndege hiyo alikuwa mhudumu mmoja ambaye alisaidiwa na abiria, na mhudumu mwingine alifungua mlango wa adharura ambapo abiria 24 waliokolewa kwa msaada wa wavuvi waliofika eneo hilo baada ya dakika tano.
View all 32 comments
23 HOURS AGO
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad