RAIS Samia Suluhu Hassan amekasirishwa na ongezeko la fedha za kununulia ndege mpya ya mizigo ya Air Tanzania kinyume na makubaliano ya awali.
Akizungumza mara baada ya kupokea ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Salum Hamduni, Rais Samia alionesha kukasirika na kudai kuwa mradi wa kutengeneza ndege ya mizigo, ambayo serikali inakaribia kuipokea last installment (malipo ya mwisho) ilikuwa illipe dola milioni 37.
“Invoice imekuja tunatakiwa kulipa dola milioni 86 …unauliza mkataba ulisemaje? Hii imetokea wapi? Ohoo vifaa vimepanda bei, vipi mkataba wetu ulisemaje?
“Bado aliyepokea anakuletea serikali hii ilipwe ndio invoice tumepokea… ‘stupid’, ulipokea umechukua hatua gani, umeuliza? Umefanya nini ukilitazama kwa undani hili ongezeko limeanzia huku ndani kuna watu wameongea huko,” alifoka na kuongeza:
“Hatuwezi kwenda hivyo nadhani hawa wanaopokea hizo invoice wakazileta kwa raha zao kabisa serikalini watupishe, hawafai kuwa kwenye hizo nafasi kama wanafaa angepokea huko akahoji.
“Baada ya kuhoji akasema nilipokea hivi, nimeambiwa hivi, lakini bado nimeomba tufanye hivi huyu unamuelewa, lakini mtu anapokea kwa raha zake tu analeta serikalini kuna hiyo ‘invoice’ imekuja vifaa vimeongezeka baada ya covid.. pumbavu haiwezekani, mawaziri tusaidieni ‘over invoicing’ zipo nyingi sana.”
Hata hivyo Rais Samia ameishukuru Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kuweza kuokoa Sh bilioni 248.45.
“Niwashukuru Takukuru, mliweza kuokoa baadhi ya fedha, mikataba mingi mibovu inaingiwa huko, ukiwaita kuwauliza kipengele hiki kwa nini ulikisaini wanabaki kutoa macho tu….mikataba ya hovyo kabisa, watu wanajiingilia tu, Takukuru endeleeni na hiyo kazi na huko ndiko kwenye upigaji.