Saraphina Avunja Ukimya Kumuiga Vanessa MDEE Kuimba "Hata Akirudi Simuogopi"


Tangu aingize mguu wake kwenye kurasa za ramani ya Bongo Fleva, Mwanamuziki Phina amekuwa akifananishwa kiumbaji na styles kama Vanessa Mdee ambaye kwa sasa ameupa Muziki kisogo.


The Melanin Queen ambaye ameachia hat-trick ya nyimbo Tatu (3.3.3) alifanya mahojiano na Kituo cha EATV, kwenye FNL ambapo aliulizwa kuhusu nafasi yake kama leo Vee Money anaamua kurudi tena kwenye Muziki


“Nafasi yangu haiwezi kuyumbishwa na mtu yeyote, yeye [Vanessa] ana nafasi yake na mimi nina nafasi yangu kwenye Muziki. Kwa hiyo I respect her na vitu alivyofanya, akiamua kurudi nitapenda kufanya naye kazi.


Lakini siwezi kutishika kwamba nafasi yangu itakuwa hatarini, hapana.” alisema Phina.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad