Serikali Kujenga njia Maalum Kupanda Mlima Kilimamjaro



Serikali imesema inatarajia kujenga njia mpya ya kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia Kidia ambayo itatumiwa na watalii maalum na wenye kipato kikubwa ili kufungua fursa za uwekezaji.


Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Uhifadhi (TANAPA), Dkt. Noelia Myonga amesema tayari shirika limepokea fedha za kutekeleza mradi huo ambapo hatua za ujenzi zimeanza ikiwemo ununuzi wa vifaa.


“Njia hii inatarajiwa kuwa na urefu wa kilometa 38 na itatumika na wasanii na watu maarufu, na ikikamilika itafungua fursa za uwekezaji na kuongeza pato la taifa,” amesema.


Aidha, Dkt. Myonga ameeleza kuwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita kumekuwa na ongezeko la idadi ya watalii wa ndani kutoka 510,000 mwezi Julai 2021 hadi kufikia 625,510 mwezi Juni 2022, akidai ongezeko hilo limechangiwa na jitihada za Serikali za kutangaza vivutio vyake ikiwemo filamu iliyoandaliwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya ‘The Royal Tour

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad