Serikali: Ugonjwa ulioua Kagera ni virusi vya 'Marburg"



Serikali imetangaza mpaka sasa ugonjwa ulioripotiwa Machi 16, 2023 kutoka Wilayani Bukoba, umejulikana kuwa ni virusi vya 'Marburg' na hadi wakati huu tayari umekwishaua watu watano huku walioathirika wakiwa ni 8 na watatu kati ya hao wanaendelea na matibabu.


Akizungumza na Wanahabari, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kwamba ugonjwa huu ambao kwa mara ya kwanza uligundulika huko Mji wa Marburg chini Ujerumani.


Akizungumzia kuhusu uambukizaji wa ugoonjwa huo, Waziri amesema "Ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine ambapo, kama utashika maji maji pale ambapo pana uwazi au mtu ana michubuko ama kidonda, na maji maji hayo yanaweza kuwa Damu, mate, mkojo, machozi yatokayo kwa maiti ama kwa mgonjwa mwenye dalilili ya ugonjwa huo"


Mpaka sasa Serikali imedhibiti ugonjwa huo kusambaa kutoka nje ya wilaya, na kwamba tangu wagonjwa waliporipotiwa Bukoba mpaka sasa haujavuka kwenda sehemu nyingine.


Aidha Shirika la Afya duniani (WHO) limeeleza kwamba ugonjwa huu si mara ya kwanza kutokea Afrika na kwamba miaka ya 2014 na 2017 umeshawahi kutokea katika nchi jirani ya Uganda

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. Asante sana kwa Taarifa Muhimu sana kwa afya ya JAMII Zetu,Kwa Pamoja tunaweza Kuzuia Ugonjwa huu wamarburg

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad