Jaji Asenath Ongeri kutokea Mahakama ya juu nchini Kenya katika uamuzi kuhusu mgogoro wa ndoa, amesema hata ikiwa Mwanaume au Mwanamke atathibitisha kwamba alipata Mtoto na Mwenza wake, haiwezi kuwa kigezo cha kuthibitisha kuwa wawili hao walikuwa wamefunga ndoa.
Katika kesi hiyo, Mwananke aliyepewa jina la FCR alisema kuwa aliishi na Mwanaume aliyeitwa CAL kati ya mwaka 1970 na 1990 na wawili hao walibahatika kupata Watoto watano.
Mwanamke huyo alidai kwamba Mwanaume alimfukuza kwenye ‘nyumba yao ya ndoa’ bila kujali kitu chochote kisha akachukua maamuzi ya kuibomoa nyumba hiyo na kuoa Mke mwinginr ili kuthibitisha kuwa kulikuwa na ndoa, Mwanamke huyo aliiomba Mahamama iamuru kifanyike kipimo cha DNA kwa Watoto wake watano pamoja na Baba yao.
Mwanamke (FCR) alidai kuwa alitoa mchango mkubwa katika harakati za kuchuma mali za familia kwa kujishughulisha na kulima, kupalilia na kutunza mashamba ya chai jijini Kericho na pia kwenye kununua nyumba na mashamba mengine pindi Baba wa Watoto wake alikuwa amesafiri kikazi, kwahiyo Mwananke huyo alisema alikuwa na haki ya kupata maslahi ya uhakika katika mali zilizochumwa, Mwanaume (CAL) alikana kila kitu akisema hakuwahi kuishi na Mwanamke huyo, kupata nae Watoto na pia hakukuwa na ndoa yoyote yakimila iliyofungwa.
Aliiambia Mahakama kuwa alioa Mwanamke mwingine aliyeitwa ICL na walikuwa na Watoto saba, Hakimu aliitupilia mbali kesi hiyo huku akisema hakuweza kuthibitisha kuwepo kwa ndoa hiyo kwa kutumia Watoto kama ushahidi na kusema ushahidi wa DNA hutumika kwenye kesi za mirathi na lakini sio katika migogoro ya mali za ndoa.