Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Kuishitaki Airbus Kwa Kuwapa Hasara


Sakata la ndege mbili za Airbus A220 za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutofanya kazi limefika katika Shirikisho la Mashirika ya Ndege Afrika (AFRAA) ili kupatiwa ufumbuzi.

Hayo yamejiri baada ya ndege hizo kushindwa kufanya kazi tangu Oktoba mwaka jana kutokana na sababu za hitilafu ya injini huku kampuni iliyotengeza ndege hizo kushindwa kuwa na injini za ziada na kupelekea hasara kwa wateja wake ikiwemo ATCL.

Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi amebainisha kuwa wanaendelea kuwabana watengenezaji wa ndege hizo kwa kushirikiana na mashirika mengine barani Afrika zenye umiliki wa ndege za aina hiyo.

“Kwa kweli hili ni tatizo, lakini tunaendelea kuwabana, kwa sasa tunashirikiana na mashirika mengine yanayotumia ndege kama hizo, likiwemo la Air Senegal, Misri kututatulia tatizo hili kwa haraka,” amesema.

Aidha, amesema watengenezaji hao wanatakiwa kuwalipa ATCL fidia ambayo ipo kwenye mkataba, “lakini imechukua muda mrefu sasa, na sasa imekuwa si suala la fidia bali wameharibu biashara na kulifanya shirika kupoteza mapato.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad