Simba: Hatuwezi kufanya kiingilio bure



Msemaji wa Simba, Ahmed Ally amesema klabu hiyo haiwezi kufanya kiingilio bure katika mechi ya hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya Machi 18 ambayo ikishinda itafuzu hatua ya robo fainali.

Ahmed amesema kuna sababu mbili za kutofanya kiingilio bure kuwa ni moja, Simba ishajaza uwanja wa Mkapa kwa kiingilio ili watu waje uwanjani na pili klabu hiyo ina mtaji mkubwa wa watu.
Amesema amepata meseji nyingi za watu wakishawishi iwe bure wakitolea mfano mechi ya Mamelodi dhidi ya Al Ahly ambayo walishinda mabao 5-2 ambalo ametolea ufafanuzi.

"Mamelodi haina mashabiki ni timu ngeni Afrika Kusini hiyo haiwezi kufanywa na Kaizer au Orlando sababu wana mashabiki wa kutosha," amesema Ahmed

Ametaja sababu nyingine ni kuwa wakifanya mechi hiyo muhimu kuwa bure mashabiki watahoji kwanini mechi za Ligi Kuu ziwe na kiingilio.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad