Tanasha Donna Afichua Ishu Ya Kuchumbiwa Baada Ya Kuondoka Nyumbani Kwa Diamond



Mwimbaji wa Kenya, Tanasha Donna amefichua kwamba ameombwa ndoa na mwanaume ambaye hajamuweka wazi.

Katika moja ya posti zake za hivi karibuni kwenye Mtandao wa Instagram, mpenzi huyo wa zamani wa staa wa muziki wa nchini Tanzania, Diamond Platnumz alidokeza kwamba huenda akakubali kuolewa na mtu huyo ambaye hajajulikana.

Tanasha Donna hata hivyo alimtaka mtu huyo amsubiri kwanza amalize kutia saini kwenye mkataba wa mamilioni.

“Naweza kusema NDIYO kubwa kwako, lakini ngoja kwanza nisaini mkataba huu wa dola milioni 1.5 Inshallah,” alisema.

Mama huyo wa mvulana mmoja wa miaka minne hata hivyo, hakutoa maelezo zaidi kuhusu taarifa hiyo yake.

Mapema mwezi huu, Tanasha alionekana kwenye jumba la kifahari la mzazi mwenzake, Diamond Platnumz jijini Dar es Salaam.

Katika video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, mwanamuziki huyo alionekana akiwa amepumzika kwenye kochi nyumbani kwa Diamond pamoja na mwanawe, Naseeb Junior.

Hiyo ilikuwa ni safari ya kwanza kwa Tanasha kwenda nyumbani kwa staa huyo wa Bongo takriban miaka mitatu baada ya kutengana kwao.


Tanasha pia aliweza kuungana na familia ya Diamond baada ya miaka mingi bila kuwaona pamoja.

Katika msururu wa video zilizopostiwa na Diamond, bosi huyo wa Lebo ya WCB alionekana akimbadilisha nguo mtoto wake huyo.

Baadaye, wawili hao walishiriki wakati mzuri wa baba na mwana ambapo Diamond alisikika akimfundisha mtoto huyo wa miaka minne jinsi ya kusoma na kutambua wanyama tofautitofauti na sauti zao.

Diamond na Tanasha walitengana mwaka wa 2020 baada ya kujaaliwa mtoto wao Naseeb Junior. Tangu wakati huo, wamekuwa wakishirikiana katika malezi huku wakiwasiliana mara kwa mara kuhusu suala hilo.

Akizungumza kwenye mahojiano mwaka jana, Tanasha aliweka wazi kuwa hakuwa kwenye mahusiano yoyote wakati huo.

Mzazi mwenza huyo wa Diamond pia alidokeza kwamba alikuwa tayari kumpa mwanaume mwingine nafasi katika moyo wake.

“Nipo single! Labda kuna mtu ambaye anaweza kuwa mpenzi anayefuata, inaweza kuwa,” alisema mwezi Julai.

Mama huyo wa mvulana mmoja alibainisha kuwa hazingatii sura ya mwanaume wala utajiri wake anapotafuta mchumba.

Alifichua kuwa jambo la msingi analozingatia kwa mwanaume anayekusudia kuchumbiana naye ni tabia yake.

“Tabia ni muhimu sana kwangu. Ni ufunguo wa kila kitu maishani kwa sasa kando na Mungu, mimi ni muumini pia,” Alisema.

Tanasha pia alidokeza kuwa mwanaume anayetazamia kuchumbiana naye ni sharti awe mwenye bidii na Mcha Mungu.

Pia alisema ni sharti mwanaume ambaye anamchumbia awe na maono kadhaa anayolenga kutimiza maishani mwake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad