Tessy "Natamani Sana Kuolewa ila Jamani Wanaume Changamoto"


Msanii wa filamu Tessy amefunguka kwa kudai kamba anatamani kuolewa ila changamoto ni wanaume ambao anakutana nao katika maisha yake.



“Plan ninazo lakini watu ambao tunapangana nao plan ndio changamoto,” Tessy ambaye ni Mama wa mtoto mmoja aliyezaa na muimbaji Aslay, alimwambia Wema Sepetu kupitia kipindi cha Cook With Sema Sepetu.

Mrembo huyo amesema anatamani kuolewa na mwanaume ambaye atakuwa na tabia kama za kwake.

“Mume Wangu natamani awe ana fanana na mimi,” Alisema Tessy “Mimi ni mpole katika mahusiano, msikivu. Nasamehe haraka hata vitu vikubwa au vyakijinga. Kwahiyo nikiishi na mtu ambaye anabebana na vinyongo inawezaikawa changamoto kwangu, kwahiyo nataka mtu ambaye ataendana na mimi,”.

Kuhusu Baba mtoto wake msanii wa muziki, Aslay ambaye alikuwa naye kwenye mahuasinao kwa miaka 3 na kupata mtoto mmoja, Tessy amedai wote walikuwa ni chanzo cha wao wawili kuachana na kubaki kulea mtoto wao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad