Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku huu wa Machi 17 katika maeneo mbalimbali nchini.
TMA imeyataja maeneo yatakayokuwa na hali ya mawingu, mvua pamoja na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua kuwa ni Mikoa ya Kigoma, Rukwa, Katavi, Mwanza, Shinyanga, Kagera na Geita.
Mikoa ya Mara, Simiyu, Tabora, Songwe, Njombe, Mbeya, Ruvuma na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Maeneo ya Dar es Salaam, Tanga, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Dodoma, Singida, Iringa, Arudha, Kilimanjaro, Manyara, Mkoa wa Pwani ukikumuisha Visiwa vya Mafia na Visiwa vya Unguja na pemba, yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua.
Mikoa ya Mtwara na Lindi inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Kwa taarifa zaidi na kwa viwango vya joto katika maeneo mbalimbali nchini, tazama hapa chini.