Uganda walianza mapema kuwekeza kumtengeneza mchezaji ambaye anakuja kushindana kwenye soko. Kwetu wachezaji wengi wameibuka kwa sababu tu ya vipaji vyao lakini wanakosa misingi imara.
Kwa hiyo mara nyingine inatokea uwanjani wote wanaonekana wapo sawa lakini hizo details ndogondogo ndio zinakuja kuamua matokeo.
Uganda wana timu ya muda mrefu, hawaiti kikosi kwa ajili ya mashindano. Timu ya CHAN inajulikana na ikija AFCON na Kombe la Dunia wanayo timu. Unaweza kuikuta timu ya Taifa ya Uganda ni ileile kwa zaidi ya miaka mitano (5) lakini kwa Tanzania ni tofauti ndani ya miaka mitano wanaweza kupita wachezaji zaidi ya 150!
Uganda huwa wanatumia michuano ya CHAN na Challenge kujenga timu yao ya Taifa, mchezaji ambaye anaonekana anafanya vizuri anapewa michuano ya CHAN lakini ni wachezaji wachache wanaopita moja kwa moja kwenda senior team kucheza mechi za kufuzu AFCON na Kombe la Dunia.