Urusi yaingilia kati sakata la ushoga Kenya, yaonya umagharibi




Kufuatia mvutano ulioibuka nchini Kenya kati ya Mahakama Kuu nchini humo na Serikali, baada ya Mahakama kuruhusu kundi la mashoga kusajili Shirika lisilo la Kiserikali (NGO), Urusi imetoa ujumbe ikikosoa kitendo hicho.

Jana, Rais William Ruto alitoa msimamo wake akieleza kuwa ingawa anaiheshimu Mahakama, suala la ushoga halikubaliki katika ardhi ya nchi hiyo.

Ubalozi wa Urusi nchini Kenya umezitupia lawama nchi za Magharibi kwa kushinikiza ajenda zinazokinzana na tamaduni na mila za nchi nyingine.

“Hali hii inaanza pale tu ambapo mataifa ya Magharibi yanapotaka kurejea kuchukua zaidi. Thamani ya mila na desturi lazima zilindwe, vinginevyo, ubinadamu unaharibiwa. Hakuna kuwa na mzazi 1 na mzazi 2, bali iwe familia! Sio muongozo, bali iwe sheria,” tafsiri isiyo rasmi ya ujumbe wa ubalozi wa Urusi nchini Kenya.


Ujumbe huo umeonesha kuunga mkono kauli za Rais Ruto na Makamu wa Rais, Rigathi Gachagua, kupinga vikali uamuzi wa Mahakama Kuu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad