Wafanyabiashara Kenya Waandamana Kupinga Wachina Kuuza Bidhaa bei ya Kutupa, China Square Yaleta Balaa

 

Wafanyabiashara Kenya  Waandamana Kupinga Wachina Kuuza Bidhaa bei ya Kutupa, China Square Yaleta Balaa

Baadhi ya Wafanyabiashara jijini Nairobi nchini Kenya wameandamana kupinga duka jipya la rejareja linalomilikiwa na raia wa nchini China, kuuza bidhaa kwa bei ya chini.


Wafanyabiashara hao, wamesema wamekasirishwa na duka hilo jipya la reja reja la China Square lililofunguliwa nje kidogo ya jiji la Nairobi, ambapo bei za bidhaa za kila siku zilizoingizwa kutoka China, huuzwa kwa bei nafuu ya wastani wa asilimia 50 kuliko bidhaa za ndani.

Kufuatia kitendo hicho, wataalamu wanaonya kuwa maandamano haya yanaweza kuwa na athari hasi kwa dhana ya uhuru wa kufanya biashara ulimwenguni na yanajiri siku moja kabla ya mkutano wa wafanyabiashara hao na Naibu Rais Rigathi Gachagua.


Mkutano huo unalenga kujadili ongezeko la wageni kufanya biashara nchini Kenya hasa raia wa kutoka Pakistan na Wachina, ambapo Wafanyibiashara wanahisi kuwa soko lao limetekwa nyara na wageni.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad