Wakala wa Adebayor afichua siri nzito Niger Mchezaji wake Kushindwa Kuja Kucheza Simba

 


Wakala wa Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Niger Victorien Adebayor amefunguka kwa mara ya kwanza namna alivyojitahidi kuhakikisha mchezaji wake anacheza soka la Bongo msimu huu 2022/23.


Adebayor alionesha kiwango kikubwa akiwa na US Gendamarie ya nchini kwao Niger, wakati ikishiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu uliopita, akifunga mabao sita.


Wakala wa Mshambuliaji huyo amesema dhamira yake kubwa ilikua ni kufanya Biashara na Simba SC ya Tanzania ambayo ilionesha nia ya kumsajili, lakini Shirikisho la Soka nchini Niger liliingilia kati na kumpeleka RS Berkane ya Morocco.


Robertinho anavyoumiza kichwa Simba SC

Amesema Shirikisho la Soka la Niger kupitia kwa Rais Djibril Hima Hamidou, lilifikia hatua ya kufanya udanganyifu ambao hakutaka kuuweka wazi, ili kufanikisha Adebayor anatimkia Morocco.


“Nilitaka kumleta Victorien Adebayo Tanzania acheze Simba SC lakini Rais wa shirikisho la soka la Niger alifanya udanganyifu, walichukua za pesa za Berkane halafu hivi sasa wamemucha kijana anahangaika peke yake, nina niwezalo kumuondoa kijana RS Berkane.” amesema wakala wa Adebayor

Tangu Adebayor asajiliwe RS Berkane mwanzoni mwa msimu huu 2022/23 ameshindwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza moja kwa moja.


Taarifa zinaeleza kuwa Adebayor kwa sasa hana furaha ndani ya klabu hiyo, na amekuwa akishinikiza kutaka kuondoka mwishoni mwa msimu huu

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad