Watanzania wapigwa ''Stop' kwa Afrika Kusini



Watanzania waishio Afrika ya Kusini wameonywa kutoshiriki kwa namna moja ama nyingine i na maandamano yanayoendelea katika nchi hiyo na badala yake wafuate sheria na taratibu za nchi hiyo.
Akizungumza kwa njia ya simu katika kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio, Balozi Meja Jenerali  Gaudence Milanzi, amesema maandamano hayo yaliyoitishwa na Chama kikuu cha Upinzani (EFF) cha nchini hiyo ya kumtaka  Rais wa nchi hiyo kujiudhulu  hayawahusu.

Akielezea sababu ya maanadamano, Balozi Milanzi ameweka wazi  ingawa hali ya uchumi nchini Afrika Kusini haipo vizuri, lakini mambo ya siasa pia yanachangia kwakuwa  uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ni mwaka ujao hivyo kinachotengenezwa ni upenyo wa kufanya siasa kwa kutumia maandamano.

"Ni kweli hali ya maisha hapa sio nzuri sana , lakini pia kuna mgao wa umeme, sasa kwenye siasa ukiacha upenyo kidogo watu watatumia kama fursa.  Maandamano haya yamepewa jina la 'National Shut down ikiwa ni pamoja na watu kumtaka Rais Cyril Ramaphosa kujiuzulu kwa sababu ya hali ya uchumi pamoja na mgao wa umeme na mengineyo kama hayo”.

Ameeleza pamoja na kwamba maandamano ya amani nchi Afrika ya Kusini wanayatambua, waandamanaji wamepewa onyo la kutowalazimisha watu wengine kuandamana ka kuwazuia kwenda kufanya shughuli zao za kiuchumi ndio maana vyombo vya usalama vipo makini katika kusimamia hilo halifanyiki.


Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote kama kuna athari imetokea kwa mtanzania yoyote, na kwamba bado wataendelea kufuatilia  kujua hali za usalama wa Watanzania.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad